Watoto mapacha Maria na
Consolata Mwakikuti (20) waliofariki mwishoni mwa wiki iliyoisha wataendelea
kukumbukwa na mamia ya walimwengu nchini kwa kuweza kuyakubali maumbile yao
waliyokuwa nayo na kujikubali mpaka kufikia hatua ya kufariki wakiwa katika mwili
mmoja.
Miaka 22 iliyopita, familia ya
Alfred Mwakiuki na Naomi Mshumbusi ilifanikiwa kupata watoto mapacha ambao ni
Maria na Consolata lakini hawakuwa pacha wa kawaida kama jamii ya kitanzania
ilivyozoea kuziona au kujaliwa nazo kwa kuwa wao walikuwa wameungana na kwa
wakati huo hapakuwepo na uwezekano wa kuwatenganisha.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu
za kuaga miili ya mapacha hao Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma
amesema vifo vya pacha hao vinafaa kutumiwa na watanzania kukumbushana wajibu
wao kwa watu wenye ulemavu.
Mbali na Askofu Maluma, naye Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema mkoa wa Iringa umepata pigo kubwa la
kuondokewa na pacha hao waliokuwa na upendo wa dhati na wenye kujitambua.
"Katika mkoa wa Iringa tumepata
mtihani wa kuondokewa na watoto waliokuwa na upendo sana, najua kwa jinsi gani
tulivyokuwa tunawapenda lakini Mungu amewapenda zaidi. Maria na Consolata
walijitambua na wakakubali maumbile waliokuwa nayo halafu wakajiamini ndio
maana waliweza kusoma kwa bidii na kufiki hatua ya chuo kikuu", amesema Masenza.
Pamoja na hayo, Masenza ameendelea
kwa kusema "niwaombe wazazi kwamba serikali ipo tayari
kuwasaidia watoto wenye ulemavu hakuna haja ya kuwaficha, waacheni watoto waje
maana neema yao ipo. Kuwaficha huko ni kutenda dhambi".
Maria na Consolata walizaliwa
Novemba 19, mwaka 1997 ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa miili yao
na kupelekea leo hii kuzikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili
katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo.
Maria na Consolata watakumbukwa kwa hili
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment