Mkuu wa Shirika la Masista la Maria
Consolata, Jane Nugi alisema malezi ya pacha walioungana, Maria na Consolata
Mwakikuti, yamesimamiwa na Mungu
Akizungumza leo Juni 6 wakati wa ibada ya
mazishi yao, Ngugi amesema tangu walipozaliwa wamepita katika mikono ya watu
wengi waliochangia ndoto zao kufikiwa
Amesema waliwalea kwenye misingi ya kumcha
Mungu, kujiamini na kuona kuwa hakuna kigumu mbele yao
Huku akiwatambulisha wengine walioshiriki
kwenye malezi ya pacha hao
“Baada ya kuzaliwa tuliamua kuwapa majina ya
Maria na Consolata kutokana na namna walivyozaliwa,” amesema
Akitoa salam za familia ya Mshumbusi, Mjomba
wa Maria na Consolata, Elisha Mshumbusi amesema kuna wakati walitoweka kwenye
malezi ya mapacha hao lakini Masister wa Shirika la Maria Consolata na Albetina
Mbilinyi waliwasaidia
Amesema japo walikuwa na ulemavu lakini
pacha hao walijaa tabasamu usoni na moyoni
"Ni pigo lakini tunalo la kujifunza,
asante sana kila aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine kwa malezi yao mapacha
wetu," amesema Mshumbusi.
Malezi ya Maria na Consolata, yalisimamiwa na Mungu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment