Magufuli atoa maagizo kwa wadau wa usalama

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewataka wadau wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti ajali za barabarani

Hayo yameelezwa na Rais katika taarifa iliyotumwa na Ofisi ya Mawasiliano ya Ikulu leo Juni 6 ambapo pamoja na mambo mengine, Rais alituma salamu za rambirambi kwa wote waliopoteza ndugu, jamaa au rafiki katika ajali ya basi na treni iliyotokea Kigoma

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika kijiji cha Gungu, Kigoma mjini baada ya basi la abiria Prince Ramida, kuigonga treni na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine 26 kueruhiwa

“Kwa mara nyingine tumewapoteza ndugu zetu 10, tumepoteza wapendwa wetu na tumepoteza nguvu kazi kubwa ya kitaifa, nawakumbusha wadau wote wa usalama barabarani, kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi.” amesema Rais
Magufuli atoa maagizo kwa wadau wa usalama Magufuli atoa maagizo kwa wadau wa usalama Reviewed by KUSAGANEWS on June 06, 2018 Rating: 5

No comments: