Watu saba wamekufa na wengine 20 kujeruhiwa leo saa 12
asubuhi baada ya basi walilopanda kugonga treni ya mizigo eneo la Gungu mkoani
Kigoma
Akiongea Kamanda wa polisi mkoani humo, Martin Otieno
amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Prince Amida kutozingatia
alama za barabarani
“Ni kweli ajali imetokea leo asubuhi. Tupo eneo la tukio
hapa kwa taarifa za awali watu saba wamefariki hadi sasa na wengine ishirini
kujeruhiwa ila bado tunaendelea kuokoa miili mingine tutatoa taarifa zaidi
baadae,” amesema Otieno
Otieno amesema dereva wa basi hilo ambalo hufanya safari zake
kati ya Kigoma kwenda Nzega mkoani Tabora amefariki na mkono mmoja
umekatika
Basi lagonga treni, saba wafariki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment