"Ni
mashujaa wa taifa letu" hiki ndicho alichosema Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili
ya pacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti
Akizungumza
leo Juni 5 mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya pacha hao,
Profesa Ndalichako amesema mashujaa hao wameliacha taifa katika simanzi nzito
"Mara ya
mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno
lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.
Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu
waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo
“Lakini kubwa
wametufundisha umoja na upendo. Wamekuwa pamoja kwa miaka 21," amesema.
Ndalichako: Maria na Consolata ‘mashujaa wa taifa’
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment