Miili ya pacha
walioungana Maria na Consolata imewasili kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha
Katoliki Ruaha Iringa (Rucu).
Tukio la
kuagwa kwa pacha hao limetangazwa kuwa ni la kitaifa na Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Richard Kasesela ameeleza kuwa Rais John Magufuli ni miongoni mwa
walioguswa na kuhuzunishwa na vifo hivyo.
"Huu ni
msiba wa kitaifa Rais angehudhuria ila amebanwa na ratiba Waziri wa Elimu, Profesa
Joyce Ndalichako na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Sera, Bunge na
Walemavu, Stella Ikupa wataudhuria hapa," amesema Kasesela
Mkurugenzi wa
Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru ni miongoni mwa watu waliohudhuria akaeleza
kusikitishwa na vifo hivyo kwa kuwa vimezuia pacha hao kutotimiza ndoto zao za
kuwa wanataaluma.
Anatumia
nafasi Hiyo kuwasihi wanafunzi kutambua mikopo inayotolewa ni rasilimali
muhimu, Serikali inalenga kuwawezesha ili wawe wataalam watakaosaidia nchi
Pacha walioungana Maria, Consolata waanza kuagwa Iringa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment