Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Ndg.
Humphrey Polepole ameonyesha Vongozi wa vyama vya Upinzani nchini, Mbowe pamoja
na Zitto Kabwe baada ya kukubaliana kushirikiana kumpata Mbunge jimbo la
Buyungu lililoachwa wazi na Mwl. Kasuku Bilago kwa kuwaambia wembe wa CCM ni
ule ule.
Polepole amesema hayo ikiwa zimepita
siku kadhaa baada ya mazishi ya Mwl. Kasuku Bilago kuzikwa huko Kakonko mkoani
Geita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kisha kwenda kuzikwa huko kijijini
kwao.
Polepole amesema kuwa "Nimesikia
jamaa palepale msibani walianza kugawana ubunge na kuanza kujihadaa, ni bahati
mbaya sana. Utamaduni wa kiafrika ni kumaliza msiba ambapo lengo ni kufariji
wafiwa".
Ameongeza kuwa "Nimekaa Kakonko
kwa muda wa kutosha, kwakuwa mmeanza siasa msibani, CCM tunasema wembe ni
uleule".
Wakiwa kwenye mazishi ya Mwalimu
Bilago ambaye alikuwa Mbunge kupitia CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Mbiowe
walikubaliana kuweka umoja ambao utamsimamisha mgombea mmoja anayekubalika
kutoka upinzani na kuhakikishia wanampigani hadi anashinda ili kumuenzi mwalimu
Bilago.
Polepole awasikitikia Zitto na Mbowe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment