Mwanaume mmoja Nchini Uganda
aliyetambulika kwa majina Joseph Ojur mwenye miaka 52 mkazi wa ukanda
wa Kabagu katika manispaa ya Njeru amejinyonga mpaka kufa baada ya
kunyimwa ‘unyumba’ na mkewe.
Kamanda wa Polisi eneo la
Njeru, Christopher Tuhunde amesema kuwa, marehemu alijinyonga ndani ya
nyumba yake na jeshi hilo linaendelea kuchunguza kwa undani juu ya tukio hilo
ili kuja na ripoti kamili kuhusiana na kujinyonga kwa Ojur.
“Naomba niwashauri ndugu zangu kuwa
muwazi na penda kuomba ushauri kwa majirani juu ya matatizo
yanayowakabili kuliko kukimbilia kujiua”, amesema Kamanda Tuhunde
Taarifa za awali zinasema kuwa
mwanaume huyo alifanya vipimo vya afya yake na kugundua kuwa na maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi ndipo mkewe alianza kumkatalia kufanya naye tendo la ndoa.
Ajinyonga kwa kukataliwa tendo la ndoa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment