Odinga apeleka salamu za Magufuli Kenya


Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga amesema Rais John Magufuli amempa salamu kwa ajili Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.

Akizungumza leo Ijumaa Juni1, 2018 katika maadhimisho ya miaka 55 ya Madaraka Day, Odinga amesema alipigiwa simu na Magufuli aliyempa salamu hizo, bila kueleza kwa kina

“Kwanza nimeleta salamu kutoka kwa rafiki wa Wameru Rais jirani wa Tanzania Mheshimiwa Magufuli, wengine mnakumbuka nilimleta Magufuli hapa wakati tunazindua ujenzi wa barabara ya Meru leo asubuhi amenipigia simu kwamba nikifika nilete salamu kwa Rais Uhuru,” amesema.

 Katika hatua nyingine amewataka raia wa nchi hiyo kuungana na kuacha ubaguzi na ukabila, hiyo kuangalia namna watakavyoweza kusonga mbele kijamii na kiuchumi

Odinga ambaye hivi karibuni amemaliza tofauti na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema, “wakenya tuungane pamoja, tuache ubaguzi, tuache ukabila na ufisadi ili tuweze kumaliza matatizo yetu.”

“Kinamama na vijana wapate kazi na wazee mpate malupulupu. Mimi na kijana mwenzangu Uhuru tumeshikana pamoja na ndiyo maana mmeona leo hii tumekuwa pamoja hapa.”
Odinga apeleka salamu za Magufuli Kenya Odinga apeleka salamu za Magufuli Kenya Reviewed by KUSAGANEWS on June 01, 2018 Rating: 5

No comments: