Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa ahirisho la mwisho
katika kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli
inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee
Akizungumza leo Ijumaa Juni 1, 2018 Hakimu Mkazi Mkuu,
Thomas Simba ametoa ahirisho hilo la mwisho kwa upande wa mashtaka baada ya
wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita kudai kesi ilipangwa kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa, hawana shahidi ikiwa ni mara ya tatu
Baada ya kutolewa maelezo hayo, hakimu Simba alitoa ahirisho
la mwisho na kupanga kesi hiyo kusikilizwa tena Juni 29, 2018 kwa mashahidi wa
upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi
Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kufanya kosa hilo Julai 3,
2017 Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni
Anadaiwa kutamka “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe
breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Halima alifikishwa
kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Julai 10, 2017. Katika kesi hiyo mbunge
huyo anatetewa na mawakili, Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya na Hekima
Mwasipu
Kesi ya Halima Mdee yaahirishwa kwa mara ya mwisho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment