Mganga Mkuu
mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Museleta Nyakiloto amezungumzia vifo
vya pacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti, akieleza kuwa walipishana
dakika 10 kufariki dunia
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Jumapili Juni 3, 2018, Nyakiloto amesema walifariki
dunia jana saa 2 usiku katika hospitali ya mkoa wa Iringa walikokuwa wakipatiwa
matibabu
“Walikuwa na
tatizo la upumuaji. Walipishana dakika 10 kuaga dunia wakati wakipatiwa
matibabu ICU (chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum). Walikuwa
wamelazwa tangu Mei 17, 2018 walipotoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es
Salaam,” amesema
“Tangu wafike
hospitalini hapa hatukuwahi kuona wamebadilika kiasi kile.
Maria ndio
alitangulia kufariki na baada ya dakika kumi alifuata Consolata. Consolata
alipomuona Maria anahangaika na umauti kumkuta naye alihangaika na kumwambia
daktari kuwa wanakufa, baada ya muda na yeye aliaga dunia.
Maria na Consolata walipishana dakika 10 kuaga dunia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment