Binti Oyinye Aguluka ameuawa kwa
kukatwa na panga na baba yake mzazi, Cletus Aguluka, masaa machache kabla
ya harusi yake.
Binti huyo ambaye anaishi nchini
Nigeria yalimkuta masahibu hayo akiwa amelala usingizini, baada ya baba yake
aliyekuwa amelewa kuja na panga na kumshambulia.
Mama Mzazi wa marehemu
aliyetambulika kwa jina la Georgina amesema mume wake alirudi usiku
akiwa amelewa na kuwauliza watoto wake mahali ilipo tochi yake, lakini hakuna
ambaye alimjibu kutokana na kwamba walikuwa wameshaingia kulala, na ndipo
alipokuja na panga na kuanza kumshambulia binti yake huyo ambaye alitakiwa
kufunga ndoa Jumamosi hii ya Juni 2, 2018.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na wazee
wa kijiji na kupelekwa kituo cha polisi, ambako anashikiliwa mpaka sasa.
Auawa masaa machache kabla ya harusi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment