Spika wa Bunge Job Ndugai
amewataka wabunge wote wanaodaiwa na Jeshi la Kujenga Taifa wahakikishe
wanalipa madeni yao haraka iwezekanavyo kwani siku zilizotolewa zinaisha
Juni 23 Mwaka huu.
Agizo
hilo la Spika limekuja baada ya kusoma tangazo hilo la madeni leo
ambapo amesema kuna orodha ndefu ya wabunge wanaodaiwa na kwamba baadhi
yao hawana hata fedha za ziada katika posho zao wanazolipwa.
“Mtakumbuka mheshimiwa Rais alitoa agizo hilo Mei 17, aliagiza madeni
yote kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia siku hiyo, leo naomba wabunge
mlipe haraka sana madeni hayo na mwisho ni Juni 23,” amesema Ndugai.
Spika amesema orodha ya wadaiwa ipo mezani kwake na kwamba angetamani
kuwataja lakini alishapitia majina yao na amebaini baadhi yao wana
mikopo ndani ya Bunge hivyo kwenye mfuko huo hawawezi kukatwa fedha za
kulipia madeni
Mei 17 mwaka huu, Rais John Magufuli alitoa mwezi mmoja kwa taasisi
za Serikali na watu binafsi wanaodaiwa na Jeshi kuhakikisha wanalipa
fedha hizo ili ziweze kutumika kujenga viwanda vingine ambapo
alidai kutolilipa jeshi ni dharau kubwa.
Madeni ya jeshi yatua bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment