Mwenyekiti wa
Kamati Maalumu ya Bunge ya Uvuvi wa Bahari Kuu, Anastazia Wambura amesema
Serikali imepoteza Sh5.98 trilioni kati ya mwaka 2009 hadi 2017, sawa na
asilimia 14.51 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18
Pia, amesema
katika kipindi hicho Tanzania imepata hasara ya Sh3.169 trilioni kutokana na
mfumo mbovu kwenye bahari kuu
Akizungumza
leo Jumamosi Juni 2, 2018 katika makabidhiano ya taarifa za kamati mbili za
kuchunguza uvuvi wa bahari kuu na gesi, Wambura amesema hatua ya Wizara ya
Mifugo na Uvuvi kusitisha utoaji wa leseni za meli za kigeni ulisababisha
hasara ya Sh5.4 bilioni katika kipindi cha 2016/17
Amesema mbali
na hasara hiyo, Taifa limekuwa likipoteza Sh352 bilioni kila mwaka kutokana na
kuuza samaki ghafi nje ya nchi
Katika taarifa
yake hiyo, Wambura amesema hatua ya kutokuwa na bandari ya uvuvi
kumeisababishia Serikali hasara ya Sh31.2 bilioni katika kipindi cha mwaka 2009
hadi 2017
Amesema
kiuhalisia sekta ya uvuvi inaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa
nchi, lakini Taifa halinufaiki kutokana na changamoto walizobaini.
Kamati ya Bunge yagundua hasara ya matrilioni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment