Bakwata yazipiga ‘pini’ taasisi nne kujihusisha na ibada ya hijja


Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limewatoa hofu waislamu wanaotarajia kwenda kwenye ibada ya hijja, likieleza kuwa limejipanga vyema kuhakikisha upungufu uliojitokeza mwaka jana haujirudii

“Taasisi nne ambazo ni Tanzania Chartable Oraganization, Haji Khikma, Taquwa Haji Group na Almadina Social Services Trust hazitosafirisha mahujaji kwa kuwa hazijakidhi masharti yaliyowekwa. Hatutaki mambo yaliyojitokeza mwaka jana, yajirudie sasa,” amesema Sheikh Hamisi Mataka, mwenyekiti wa baraza hilo.

Mataka ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 2, 2018 jijini hapa, katika mkutano wake na waandishi wa habari, kubainisha kuwa zaidi ya mahujaji 100 mwaka, 2017  walikwama kwenda kufanya ibada hiyo baada ya taasisi ya Twaiba iliyokusanya fedha zao kwa madai ya kuwawezesha kusafiri, kuingia mitini.

 “Mpaka sasa mambo yote yanakwenda vizuri, hakuna tishio lolote ambalo tumelibani la mahujaji kutosafiri kwa sababu mambo yote yapo katika mstari kuhakikisha kuwa waislamu wanatekeleza ibada hiyo,”amesema  Mataka

Mataka amesema moja ya hatua walizozichukua ni pamoja na kutoruhusu taasisi zisizokidhi vigezo kuwadanganya tena wananchi
Mataka alisema taasisi 11 pekee ndizo zilizokidhi vigezo na msharti yaliyowekwa ikiwemo , Alhusna Haji Trust, Shamsul Maarifa Kheri na Tanzania Muslim Development Asociatiaon, Tanzania Muslim Haji Trust

Katika hatua nyingine Mataka amessema kuanzia Juni 8, 2018 waislamu nchini kupitia misikiti yao watafanya harambee ya kuchangia maendeleo ya baraza hilo ili liweze kutekeleza majukumu yake mbalimbali, ikiwemo kuwalipa watumishi.
Bakwata yazipiga ‘pini’ taasisi nne kujihusisha na ibada ya hijja Bakwata yazipiga ‘pini’ taasisi nne kujihusisha na ibada ya hijja Reviewed by KUSAGANEWS on June 02, 2018 Rating: 5

No comments: