Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya
watalazimika kupimwa kwa kutumia kifaa cha kuwafichua watu waongo ikiwa ni
miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi.
Akihutubia makundi ya raia
waliokutana kusherehekea miaka 55 tangu Kenya ijipatie Uhuru , amesema kuwa
Kenya italazimika kuangamiza ufisadi kabla ya jinamizi hilo kuangamiza ufanisi
na siku za usoni za vizazi vijavyo.
''Wacha nitaje mpango mmoja ambao
tunapanga kuidhinisha kukabiliana na ufisadi. Kama hatua ya kwanza , wakuu wote
wa idara za kutoa zabuni na zile za hesabu katika wizara za serikali
watafanyiwa ukaguzi mpya ikiwemo kupimwa na kifaa cha kuwatambua watu waongo
ili kujua maadili yao. Wale watakaofeli watasimamishwa kazi'' amesema.
Kenyatta ameeleza kuwa kifaa hicho
ambacho kitafichua maadili ya wafanyakazi ni miongoni mwa mikakati ya
kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo hotuba ya rais Kenyatta
ni jaribio la kukabiliana na tatizo hilo ambalo kwa limekomaa baada ya
kufichuliwa kwamba kiasi cha dola bilioni 8 za Kenya zilipotea katika kitengo
kimoja cha serikali takribani wafanyakazi 40 wa umma wanakabiliwa na kashfa
hiyo.
Kashfa hiyo ya ufisadi , ambayo
ilifichuliwa na wauzaji bidhaa ambao walikuwa hawajalipwa , ilipelekea kuibiwa
kwa fedha hizo katika shirika la vijana wa huduma kwa jamii NYS kupitia vyeti
bandia na malipo ya ziada.
Kifaa cha kuwafichua waongo chatua kwa Kenyatta
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment