Jeshi la Polisi mkoani Morogoro
linawashikilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti akiwemo mmoja kwa
kukamatwa na Pembe za Ndovu mbili za thamani ya shilingi milioni 34 na mwingine
kwa kukutwa na Katoni 56 za Vipodozi vilivyopigwa marufuku
Watuhumiwa waliokamatwa ni Joel Amos
mkazi wa Mikumi aliyekutwa na Pembe mbili za Ndovu zenye uzito wa gramu kumi,
za thamani ya shilingi milioni 34 na Bibiana Mwita mkazi wa Kitunda Dar es
Salaam aliyekutwa na Katoni 56 za vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini
ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Urlich Matei amesema kukamatwa kwa
Joel kumefanywa na polisi kwa kushirikiana na maafisa Wanyama Pori.
Wawili washikiliwa na Polisi Morogoro kwa kukutwa na Pembe za Ndovu."
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment