Serikali ya
Burundi imeungana na wanakijiji cha Ruagarika mkoa wa Chibitoke kuzika miili ya
watu 26 waliouawa kikatili kwa kupigwa risasi na maiti zao kuchomwa moto na
kundi linalosadikiwa kuwa la waasi kutoka Congo DRC
Tukio hilo limehudhuriwa
pia na mabalozi na wawakilishi wa
Jumuiya mbalimbali za kimataifa huku Mwenyekiti wabaraza la kudhubiti machafuko
nchini Burundi Bw.John Didi akilaani kitendo hicho na kutaka serikali ya
Burundi na Jumuia ya Afrika Mashariki kuhakikisha wanatokomeza vikundi hivyo
kwa maslahi mapana ya warundi na Afrika kwa ujumla.
Kwa mujibu wa taarifa ya Gavana wa
jimbo hilo watu hao waliuawa na kikosi cha Askari Jeshi waliovuka mpaka kwa miguu
wakiwa na silaha za kivita na kisha kushambulia kijiji hicho kwa kuuwa watu 26
na wengine kujeruhiwa.
iili ya watu 26 waliouawa kikatili na kuchomwa moto, yazikwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment