Serikali imesema tangu kuanzishwa kwa Bunge
la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi sasa jumla ya sheria 78 zimetungwa na kati
ya hizo sheria 20 zimeridhiwa na wakuu wa nchi wanachama huku nyingine zikiwa
zipo katika hatua mbalimbali za kusainiwa na kuridhiwa
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mh Dk. Augustine Mahiga wakati akijibu swali
la Mh Ally Salehe Mbunge wa Malindi aliyetaka kujua ni sheria ngapi zimetungwa
tangu kuanzishwa kwa umoja huo
Mh dk. Mahiga amesema sheria zilizotungwa
zimelenga katika kuimarisha biashara kukuza uchumi baina ya nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwezesha taasisi na vyombo vya jumuiya
kutekeleza majukumu yake
Sheria 78 zimetungwa tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika Mashariki.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment