Zikiwa zimepita
takribani siku 6 tokea kulipofunguliwa dirisha la uombaji mikopo kwa njia ya
mtandao nchini, wanafunzi na wadau mbalimbali wameendelea kuilalamikia Bodi ya
Mikopo kwa kuweka vigezo vigumu bila ya kuwafikilia kwa undani watu wanaotaka
kufaidika nayo.
Akizungumza kwenye kipindi cha EATV
Saa1 Katibu Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP), Joseph Malecela amesema katika
utoaji wa mikopo hiyo kumekuwa na ubaguzi wa upendeleo kwa baadhi ya michepuo
ya wanafunzi hasa hasa wanaosomea sayansi huku wengine wakikosa kabisa.
Mbali na hilo, Malecela amesema ni
vyema Bodi ya Mikopo itoe ufafanuzi zaidi juu ya kifungu cha muongozo wa kuomba
Mkopo Na 1.0 (vii) ambacho kinasema 'waombaji ambao wazazi au walezi ni
wamiliki wa biashara, mameneja wakubwa katika mamlaka zinazotambulika zenje
usajili, hawaruhusiwi kuomba mkopo'.
"Sisi tunachojiuliza kama
Mtandao wa wanafunzi Tanzania kwamba tuna mfumo gani wa mkopo ambao unaweza
kupima kiwango cha uwezo wa mzazi katika kuweza kumudu hizo gharama, na
madodoso gani yamewekwa ili kujua huyu mtu anafanya biashara kubwa hata kama si
Meneja mkubwa", amesema
Malecela.
Kwa upande wake Afisa Mawasiliano
Mwandamizi kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bi. Veneranda Malima amesema
kifungu hicho kipo sawa na hawawezi kusema kwamba kitaondolewa.
Vigezo vya mikopo chuo kikuu vyazua gumzo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment