Watu 22 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu

Watu 22 wamepoteza maisha hadi sasa, huku zaidi ya watu 710 wakiugua ugonjwa wa kipindupindu kwenye Bonde la ziwa Rukwa, katika halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, tangu ugonjwa huo ulipoibuka kwenye maeneo hayo Novemba mwaka jana

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Bw.Nyange Msemakweli,akizungumzia kuhusu ugonjwa huo unaoenea kwa kasi kwenye bonde hilo la ziwa Rukwa,amesema katika awamu ya kwanza ya ugonjwa huo ulioanza Novemba 2017, watu wanane walipoteza maisha na ugonjwa ukatoweka kwa muda wa siku 62 tu,ambapo tena umeibuka kwa kasi kuanzi Mei 6 mwaka huu,na kusababisha vifo 14 na watu 327 kuugua

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Sumbawanga Bw. Kalolo Ntilla,akiongelea kuhusu baa hilo la ugonjwa wa kipindupindu,amesema halmashauri yake imefikia maamuzi ya kuwafikisha mahakamani watendaji wa vijiji na kata pamoja na wenyeviti wa vijiji mahakamani,ambao ugonjwa huo utaibuka katika maeneo yao ili kudhibiti uzembe wa kutosimamia usafi

Watu 22 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu Watu 22 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu Reviewed by KUSAGANEWS on May 29, 2018 Rating: 5

No comments: