Nairobi,
Kenya. Jeshi la Polisi limewakamata na kuwaweka ndani maofisa wa ngazi ya juu
zaidi ya 50 na watendaji wakuu baada ya wananchi kuonyesha hasira kutokana na
madai ya wizi wa zaidi ya dola za Marekani 100 milioni katika mashirika ya
serikali
Baada ya zaidi
ya wiki ya kusoma habari nyingi katika kurasa za mbele za magazeti ya Kenya na
mitandao ya jamii, ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma ilitangaza Jumatatu
kwamba mashtaka yatafunguliwa kwa watuhumiwa wote ambao majina yao yatakuwa
katika mafaili yaliyoandaliwa na idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai
Watuhumiwa hao
ni pamoja na Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa (NYS) Richard
Ndubai, viongozi waandamizi na wanachama wanne wa familia moja, wanaohusika
katika biashara ya ufisadi
Watuhumiwa hao
kwanza walipelekwa kwenye vituo vya polisi vya Muthaiga, Gigiri na Makao makuu
kisha wakapelekwa makao makuu ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Kiambu Road, Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta, ambaye aliahidi kupambana
na ufisadi alipochaguliwa kwa mara ya kwanza 2013, haraka alichukua hatua za
kupunguza hasira za umma. “Hatutawavumilia watu wasiowaaminifu.
Watu
waliokabidhiwa majukumu lazima wawe tayari kutumikia badala ya kutumikiwa,”
alisema Jumatatu
Wakosoaji wake
wanasema, Kenyatta ambaye alishinda kiutata muhula wa pili mwaka jana amekuwa
mlegevu kuwafuatilia viongozi wa juu. Hakuna viongozi wowote wa ngazi ya juu
ambao wamechukuliwa hatua tangu alipoingia madarakani
Kashfa ya
ufisadi imezingira katika Shirika la Taifa la Huduma ya Vijana (NYS), taasisi
ya kijeshi ambayo inawafundisha vijana na kuwapeleka kwenye miradi inayoanzia
ujenzi hadi udhibiti wa usalama barabarani. Mradi huo umekuwa kipaumbele katika
mpango wa Kenyatta kukubali ukosefu wa ajira wa vijana
Mkurugenzi
mkuu wa mashtaka amesema anafanyia uchunguzi ankara mbalimbali za malipo
yanayofikia shilingi za Kenya 8 bilioni (pauni 59 milioni). Uchunguzi wa awali
unaonyesha malipo ya ankara nyingi yamezidishwa
Vyombo vya
habari vya Kenya vimeonyesha kwamba NYS lilitumia dola 10 milioni kulipia nyama
kwa mwaka mmoja ikiwa na maana kwamba kila kuruta alikuwa anakula kilo 66 za
nyama kwa siku
Ankara
nyingine, vyombo vya habari vimeandika tairi moja ilinunuliwa kwa dola 1
milioni.
Maofisa 50 waswekwa mbaroni kwa ufisadi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment