Wanawake Nchini Kenya wameandamana
leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za kufukuzwa kwa mwanamke mmoja katika
mgahawa mmoja kwa kumyonyesha mtoto wake.
Wanawake hao wameelekea katika
mgahawa wa Olive Restaurant, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa
ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye mri wa mwaka mmoja.
Taarifa hiyo imezusha hisia za watu
wengi nchini humo na kusababisha makundi ya kutetea haki za wanawake kuandaa
maandamano.
Wakina mama hao wamesema maandamano
ya leo ni kushinikiza haki za akina mama waungwe mkono na kusaidiwa katika
kufanikisha kuwanyonyesha watoto wao bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Wanawake waandamana kwa hasira
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment