Serikali kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia imesema wanafunzi wanaosoma katika shule binafasi
wataendelea kutozwa ada ya mitihani ya taifa kwa kuwa programu ya elimu bila
malipo haizihusu shule hizo hivyo wazazi na walezi ni jukumu lao kugharamia
huduma hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 15,
2018 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha Bungeni
Jijini Dodoma kwenye kikao cha 29 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge Viti Maalum Ester Mahawe
aliyetaka kujua ni lini serikali itafuta ada ya mitihani ya Taifa kwa shule za
msingi na sekondari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi ?.
"Serikali inatambua umuhimu wa
sekta binafsi katika utoaji elimu nchini. Ili kuhakikisha mazingira rafiki
katika utoaji wa elimu serikali imekuwa ikifanya majadiliano na sekta binafsi
kwa lengo la kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabiri. Katika utekelezaji
wa mpango wa elimu bila ya malipo, serikali ilifuta ada na michango ya lazima
katika shule za umma ngazi ya elimu msingi hadi kidato cha nne", amesema Olenasha
Pamoja na hayo, Naibu Waziri
Olenasha ameendelea kwa kusema "ada na michango hiyo iliyokuwa
inalipwa na wazazi au walezi kwasasa inagharamiwa na serikali, mpango huu
haujazihusisha shule binafsi pamoja na umma ngazi ya kidato cha tano na sita.
Hivyo shule hizo zitaendelea na utaratibu wa wazazi au walezi kulipa ada za
mitihani ya Taifa".
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema serikali itaendelea
kuboresha mazingira ya utoaji elimu nchini kadri uwezo wa kifedha utakaporuhusu
kufanya hivyo.
Ada ya mitihani yaibuka Bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment