Wanafunzi wawili wamekufa maji baada
ya kivuko walichokuwa wakitumia kuzama katika eneo la Chulwi wilayani Mkuranga
mkoani Pwani, huku watu wazima 10 wakiokolewa.
Kwa mujibu wa ripota wetu Ali Hengo
aliye eneo la tukio amesema wanafunzi hao walikuwa wakivuka kwenye kivuko
ambacho sio rasmi wanachokitumia kila siku kwa ajili ya kwenda shuleni
huku wakiwa na wananchi wengine, ambacho ndio kimezama na kusababisha vifo
hivyo.
"Kuna watu walikuwa wakivuka
pamoja na wanafunzi sasa wakazama, baada ya kuzama watu wazima waliokolewa
lakini wanafunzi wawili, mmoja amekutwa amekufa mwingine amezama kwenye maji na
hajulikani alipo, amesema Ali Hengo.
Ali ameendelea kuelezea hali halisi
ya eneo hilo na kusema kwamba ..."Hiyo sehemu kuna kivuko watu wanavuka
kienyeji sasa wanatumia mipira ya matairi ya gari ama miti kutengeneza
tengeneza kama vingalawa tu vidogo vya kuvuka, sasa kutokana na mvua
iliyonyesha ndio zikasababisha madhara haya".
Wanafunzi wafa maji Mkuranga, Pwani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment