Wabunge wa CCM, Richard Ndassa (Sumve) na Mashimba Ndaki
(Maswa Magharibi) wamekataa kuunga mkono bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka
2018/19, kuwashawishi wabunge wenzao wanaotoka maeneo yanayolima pamba,
kutoipitisha bajeti hiyo hadi Serikali itakapoeleza sababu za bei ya zao hilo
kushuka kutoka Sh1,200 hadi Sh1,100
Ndassa ndiye aliyeanza kuzungumza katika mjadala wa bajeti
hiyo leo Mei 15, 2018 bungeni mjini Dodoma na kubainisha, “mheshimiwa
mwenyekiti (Andrew Chenge) siungi mkono bajeti hii hadi nipate maelezo ya
kutosha.”
“Pamba ni siasa na pamba ni uchumi na nisipopata maelezo ya
kutosha siungi mkono bajeti hii. Waziri Mkuu alihamamasisha wakuu wa mikoa kumi
na wilaya 46 zinazolima pamba walime nao wakalima.”
Amesisitiza, “Wananchi wakalima kweli kweli, lakini
matarajio ya wakulima, kilo ilikuwa Sh1,200, lakini bila aibu bei ya sasa ni
Sh1,100 hivi mkulima huyu tunamsaidia namna gani? Kila msimu unapoanza bei ya
pamba peke yake, tatizo ni nini?”
Kwa upande wake Ndaki amesema bajeti hiyo hawawezi
kuipitisha kama suala la ushirika halitafanyiwa kazi kwani linawakandamiza
wakulima na kuwanufaisha wengine na kama hatutachukua hatua za haraka wakulima
hawa hawatanufaika
Mara baada ya kauli hiyo ya ushirika kuwakandamiza wakulima,
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisimama na kumpa taarifa
Ndaki kwamba baadhi ya vyama vya ushirika wamechagua viongozi wasio na sifa
katika maeneno hayo, hawaaminiki.”
Kwa upande wake, Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM), Mahmoud
Mgimwa amesema kama Serikali haitatoa majibu kuhusu Wakala wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) atawahamisiha wabunge wote wanaotoka maeneo hayo kuikataa bajeti
hiyo kama hawatapata majibu ya suala la ununuzi wa mahindi
Wabunge CCM wapania kutoipitisha bajeti Wizara ya Kilimo 2018/19
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment