Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkoga, Kitongoji cha Tambani
wilayani Mkuranga, Amiri Mbamba ameagiza wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari wanaolazimika kuvuka Mto Kizinga, kutokwenda shule baada ya mto huo
kujaa
Mbamba alitoa tangazo hilo jana jioni Mei 14, 2018 kwa
kupita katika nyumba za eneo hilo na kuwasihi wazazi wasiwaruhusu watoto wao
kutoka majumbani kwa ajili ya usalama wao
Mto Mzinga ulianza kujaa maji jana saa tatu asubuhi jambo
lililowalazimu wavushaji eneo la Bonde la Mkoga kusitisha kazi hiyo
Hata hivyo, hali ya kujaa maji iliongezeka jana Jumatatu
jioni na kusababisha sehemu ya daraja iliyokuwa ikitumika kufunikwa na maji
hayo
Tangazo hilo pia liliwagusa wavushaji ambao wametakiwa
kutovusha mwanafunzi yeyote hadi maji yatakapopungua
Watu wazima ambao walikuwa wanavuka kwenye mitumbwi
walilazimika kulipa gharama ya Sh1,500 hadi Sh2,000
Wanafunzi wazuiwa kwenda shule baada ya mto kujaa maji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment