Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu
Lulu ameanza kutumikia kifungo chake cha nje kwa kufanya usafi katika
ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma
za jamii, Charles Nzase amesema Lulu anaungana na wafungwa wengine 10
wanaofanya usafi wa mazingira wizarani hapo.
Amesema kila siku mwigizaji huyo
atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine
za ujenzi wa Taifa.
Ameongeza kuwa tayari msanii huyo
alianza kutekeleza adhabu hiyo tangu jana na kwamba ataendelea mpaka
atakapomaliza kifungo chake Novemba, mwaka huu.
“Atapumzika siku za Jumamosi na
Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo
wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira,” amefafanua Nzase.
Lulu Michael Keshaanza Kutumikia Kifungo chake cha Nje kwa Kufanya Usafi Wizarani ya Mambo ya Ndani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment