Wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga zaidi ya
3000 wamesajiliwa kwa ajili ya kupata vitambulisho vya kutambuliwa huku
wafanyabiashara 100 wakisajiliwa na kupewa vitambulisho hivyo rasmi ikijumuisha
kanda nzima ya kaskazini.
Akizungumza na wafanyabiashara hao mkuu wa wilaya ya
Arushakwa niaba ya mkuu wa mkoa Fabian daqaro amesema serikali kwa kutambua
umuhimu wa wafanyabiashara wadogo imeona ni vyema kutoa vitambulisho rasmi
kupitia TRA lengo likiwa ni kuwatambua ili waweze kuwa uhuru bila kubughudhiwa
na mtu yeyote ikiwa ni agizo la Raisi Dokta John Magufuli
Katika uzinduzi huo wa usajili wa utoaji wa vitambulisho
wasio kwenye isiyo rasmi serikali imeona ni vema kuwapa wafanyabiashara hao
kutambulishwa na kutimiza wajibu wao na kuchangia pato la taifa
Kwa upande wake kaimu kamsishna kutoka makao makuu TRA ndugu
Zuberi Abdul amesma kuwa zoezi hilo ni la kitaifa na linafanyika nchi nzima kwa
kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashar ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa
kuchangia pato la taifa kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania.
Hata hivyo amesema kuwa katika kutekeleza azma ya
serikali mamlaka kwa kushirikana na wadau wengine ambao ni mamlaka ya
vitambulisho NIDA serikali za mitaa wakala wa usajili ufilisi na Udhamini RITA
pamoja na idara ya uhamiaji imeanza kutambua vikundi mbalimbali vya
wafanyabiasharra kwa kuwapatia kitambulisho na namba ya kitambulisho cha mlipa
kodi TIN
Hata hivyo ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wadogo
walio kwenye sekta isiyo rasmi kujiunga kwenye vikundi vinavyotambuliwa
kisheria na serikali pamoja na usajili wa kurasimisha shughuli zao ili
zitambulike serikalini na wadau wengine zikiwemo tasisi za fedha.
Kwa upande wa wafanyabiashara wamesema lengo la
kuanzisha umoja wa vikundi ni ili kuomba srrikali iwapatie maeneo rasmi ya
kufanyia biashara kwani wengi wao wamekuwa hawana maeneo rasmi
MACHINGA ZAIDI YA 3000 WASAJILIWA NA KUTAMBULIWA RASMI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment