Wananchi wa vijiji 15 wanufaika na maji safi ya visima


Wananchi wa vijiji 15 vya halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wameanza kunufaika na mradi wa maji wa visima vya kupampu unaotekelezwa na Shirika la help for Under Served Community ambapo Waziri wa Sera, Bunge, kazi, ajira, vijana na walemavu, Mh. Jenista Mhagama amekabidhiwa vifaa mbalimbali zikiwemo pampu 52 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa visima hivyo kwenye vijiji sita vilivyobakia

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Waziri wa Sera, Bunge, kazi, ajira, vijana na walemavu, Mh. Jenista Mhagama ambavyo vinafanya jumla ya thamani yote kuwa Bilioni 1.7, Mkurugenzi wa uendeshaji na miradi kutoka Shirika la help for Under Served Community, Bw. Salim Abbas amesema lengo la mradi huo ni kuifanya jamii isiyojiweza inapata huduma stahiki ikiwemo maji safi na salama, elimu pamoja na afya

Hata hivyo Mh. Jenista Mhagama amesema bado kuna maeneo tete ambayo hayafikiki kirahisi hivyo ameliomba shirika hilo kuona namna ya kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo kupata maji safi na salama huku Kaimu Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Songea, Eng. Pilly Mungwana akisema ujenzi wa visima hivyo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi kutoka asilimia 59.1 hadi asilimia 60
Wananchi wa vijiji 15 wanufaika na maji safi ya visima Wananchi wa vijiji 15 wanufaika na maji safi ya visima Reviewed by KUSAGANEWS on May 27, 2018 Rating: 5

No comments: