Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema amefunguka kuwa bado wanaendelea kutafakari suala la Mbunge wa Sigida
Mashariki Tundu Lissu kuhangaika na kutafuta misaada ya matibabu kwa watu mbali
mbali duniani, kwani Bunge bado linatafakari kuhusu stahiki zake, haki na
gharama za matibabu.
Mhe. Lema amzungumzia hayo ikiwa ni
siku moja tangu kutokea kwa kifo cha Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago aliyefariki
wakati akipatiawa matibabu katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.
Lema amesema "Mwili wa
Marehemu Mhe. Bilago umepata heshima, haki na stahiki ya Kibunge, tumefanya
kikao tena Kati ya Bunge, Chama na Familia, wema wa Bunge kwa mwili wa marehemu
umekuwa ni wa kifani".
"Ameongeza "Wakati
tunalishukuru Bunge kwa wema huu, bado tunaendelea kulitafakari la rafiki yetu
Lissu aliyeko Ubeligiji".
Lissu ambaye anatibiwa nchini
Ubelgiji alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 9, 2017 maeneo ya Area
D akiwa anatokea katika majukumu yake ya kikazi bungeni Dodoma.
Sabbu za Lissu kutotibiwa na Bunge
ziliwekwa wazi na Spika wa Bunge, Job Ndugai siku moja baada ya tukio
hilo ambapo alisema kuwa utaratibu wa matibabu kwa mbunge ulikuwa umeshafuatwa
lakini familia pamoja na chama waliamua kumpeleka Nairobi, na siyo kama
wao walishindwa kumpeleka nchini India.
Lema alipongeza Bunge, akomaa na Lissu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment