Jeshi la polisi kikosi cha Usalama
barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam limekusanya shilingi 972.7 milioni za
makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha wiki mbili.
Katika operesheni hiyo ya ukamataji
wa magari iliyofanyika kati ya Mei 11 hadi Mei 24 mwaka huu ambapo magari
yaliyokamatwa ni 24,116, pikipiki 763, na daladala 10,301.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana jijini Dar es salaam, kamanda wa kanda hiyo Lazaro Mambosasa alisema.
” Waendesha bodaboda waliofikishwa
mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakia mishikaki yaani abiria
zaidi ya mmoja ni 59, jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 30,850 na fedha
zilizopatikana ni Sh972 milioni.
Ameongezea kuwa madereva na wamiliki
wa magari wanatakiwa kulipa faini zao ndani ya siku saba ili kuepuka faini
kuongezeka na kusababisha kukamatwa tena kwa kulimbikiza madeni.
972.7 Milioni zakusanywa kwa makosa ya usalama barabarani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment