Wananchi Mbulu wanatembea umbali wa Km 40 kupata huduma za afya.


Tatizo la ukosefu wa wataalumu wa afya katika hospitali ya wilaya katika halmashauri ya Mbulu mkoani Manyara imesababisha wananchi wa kata ya Yeda chini kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 40 kutafuta huduma za afya katika hosptali ya Rufaa ya haydom

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw.Hudson Kamoga amesema tatizo la ukosefu wa huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Yaeda ni kubwa hususani kipindi hiki ambacho mvua zimenyesha na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara

Amesema kutokana na ukubwa wa tatizo hilo halmashauri ya wilaya ya Mbulu inashirikiana na hospitali ya rufaa ya Haydomu kutumia usafiri wa ndege ili kutoa huduma za afya kwa njia ya kliniki tembezi  kwa wananchi wa vijiji vya wilaya hiyo ambao wanashindwa kufika hospitalini kutokana na ukosefu wa magari

Kutoka na tatizo hilo Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa ya Hayadom Dk Emmanuel Nuwas amesema msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo ni mkubwa na kwamba changamoto kubwa ni uharibifu wa miundombinu ya barabara

Baadhi ya wananchi wilaya ya Mbulu wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kusogeza huduma za afya maeneo ya vijijini pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara kutokana na wananchi kutumia muda mrefu na gharama kubwa kutafuta huduma za afya.
Wananchi Mbulu wanatembea umbali wa Km 40 kupata huduma za afya. Wananchi Mbulu wanatembea umbali wa Km 40 kupata huduma za afya. Reviewed by KUSAGANEWS on May 27, 2018 Rating: 5

No comments: