Baraza la
Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora limemsimamisha kazi
Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) wilayani humo,
Benjamini Brighton Mujuni kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya
fedha za mradi wa maji
Uamuzi wa
kusimamishwa kazi mtendaji huyo umetangazwa leo Mei 27 na mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya hiyo, Peter Nzalalila, baada ya kufanyika kikao cha
baraza la madiwani juzi Jumamosi, Mjini Sikonge
Nzalalila
amesema madiwani wamejadili kwa kina tuhuma mbalimbali zinazomkabili na
kujiridhisha pasipo shaka kuwa meneja huyo, ameenda kinyume na maadili ya
utumishi wa umma
“Serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli haitaki kusikia
ubadhirifu au uzembe wa aina yoyote ile kwa mtendaji au mtumishi wa umma, na
hii ni salamu kwa kila mtumishi kutekeleza wajibu wake ipasavyo vinginevyo
tutamwondoa,”alisema
Mwenyekiti wa
Bodi ya Suwasa, Juma Ikombola, alisema walipokea barua za malalamiko ya
kunyanyaswa wafanyakazi wake ikiwemo kutopeleka makato yao ya NSSF benki, kwa
kipindi cha mwaka mzima sasa.
Baraza la Madiwani lamsimamisha kazi meneja Suwasa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment