Wasichana 500 wa shule mbalimbali za msingi na sekondari
jijini Dar es Salaam, kesho watanufaika na taulo za kike zinazoweza kufuliwa na
kutumika tena
Ugawaji wa pedi hizo unafanyika katika maadhimisho ya siku
ya hedhi duniani kesho
Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika bwalo la maofisa wa
polisi, yanafanyika wakati asilimia 65 ya wanawake na wasichana nchini Tanzania
wakishindwa kumudu kutumia pedi katika siku zao za hedhi
Akizungumza na vyombo vya habari leo Mei 27, Mkurugenzi wa
Asasi ya Chief Promotions, Amon Mkoga amesema zaidi ya wasichana 850,000
wanakosa wiki sita za masomo kila mwaka huku wanawake wakipoteza saa zao za
kufanya kazi
“Kesho tutagawa pedi kwa watoto zaidi ya 500 wa shule
mbalimbali za msingi na sekondari, tutakuwa na pedi aina mbili ambazo ni
zile za kutumia na kufua ‘relief pad’ anaweza akavaa mwaka mzima pamoja na HQ,”
amesema Mkoga.
Amesema katika matembezi hayo ya hisani, yatakayoongozwa na
Naibu Waziri wa Afya Dk Faustine Ndugulile kutakuwa na wasambazaji wa pedi
ambao watakuwa na mabanda yao
“Tatizo ni kubwa kwa eneo lolote lenye umaskini tutazungumza
nini kinafanyika mwaka huu lakini pia kuna wadau maalum ambao wanawaangalia
watu mbalimbali wenye mahitaji maalum wanapatiwa msaada kwa mwaka mzima hawa
tutawatambua kupitia viongozi wao wa kata,” amesema
Meneja wa kampuni ya Relief Pad inayozalisha pedi za kudumu,
Sangamesh Salimaly amesema pedi hizo za kutumia na kufua zimetengenezwa kwa
malighafi maalum ambazo zinaweza kuhifadhi pasipo kuvujisha na kumfanya mhusika
awe mkavu muda wote.
“Ndani ya pikiti moja
zinakaa pedi tano, moja ni kubwa, hizi mhusika anatumia na kufua na zinaweza
kukaa kwa muda wa mwaka mzima bila kuharibika,” amesema Salimaly.
Mabinti 500 kupewa taulo za kike zinazoweza kufuliwa, kutumika tena
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment