ACT-Wazalendo kufanya uchaguzi wa viongozi kitaifa Agosti 25


Chama cha ACT-Wazalendo kitafanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa Agosti 25 mwaka huu jijini Mbeya

Akizungumza leo Jumapili, Mei 27, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu amesema uchaguzi wa ngazi za chini unaendelea hivi sasa

Viongozi wa ACT-Wazalendo waliopo madarakani walichaguliwa mwaka 2015.

Shaibu amesema baadhi ya nafasi za kitaifa zitakazowaniwa ni kiongozi wa chama,mwenyekiti,makamu mwenyekiti na katibu mkuu

"Tunaomba wanachama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.chama chetu kina demokrasia ya kweli," amesema

Amesema uchaguzi huo unafanyika ili kujiandaa na chaguzi za kiserikali

ACT-Wazalendo kufanya uchaguzi wa viongozi kitaifa Agosti 25 ACT-Wazalendo kufanya uchaguzi wa viongozi kitaifa Agosti 25 Reviewed by KUSAGANEWS on May 27, 2018 Rating: 5

No comments: