Wimbi la panya wanaoharibu mazao mashambani limeibuka kwenye
maeneo mbalimbali katika halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani ambapo zaidi ya
eka 30,000 za mahindi yameharibiwa kwa kuliwa na wanyama hao
Baadhi ya kata zinazodaiwa kuvamiwa na panya hao ni Mandela,
Bwewe, Lugoba na Kibindu na pia wanyama hao wanafukua na mazao jamii ya viazi.
Baraza la Madiwani wa
Chalinze leo Mei 27, wamemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya eneo hilo, Edes
Lukoa kuwasiliana mara moja na mamlaka husika ili kupata dawa ya kuua panya
hao.
Diwani kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya amesema panya hao
wameanza kuharibu mazao hayo tangu msimu wa vuli na sasa wameongezeka mno na
wanaonekana si wale wa kawaida waliozoeleka kuonekana hata majumbani
"Tumehamasisha wananchi walime mazao ya chakula msimu
huu kweli wamelima sana lakini cha kusikitisha mwenyekiti limeibuka wimbi la
panya wanakula mahindi na tayari zaidi ya eka 20,000 zimeliwa, mbaya zaidi hawa
panya wanakula pia na mpunga na wanafukua viazi, hali si shwari
mashambani," amesema Mkufya
Panya wateketeza eka 30,000 za mahindi Chalinze
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment