Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amewataka Watanzania
kujiepusha na vitenda au kauli zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani
miongoni mwa Watanzania
Akizungumza katika Mashindano ya kuhifadhi Quraan
yaliyohusisha nchini mbalimbali, Mhe Majaliwa amewataka kuwapuuza wale watu
wanaowapuuza watu wanaounga mkono jitihada za serikali katika kulinda
amani na kuleta maendeleo ya Watanzania
Awali akizungumza na maelfu ya waislamu walihudhuria
mashindano hayo Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zuber Bin Ali
amewataka waislamu kote nchini kujenga umoja wenye mshikamano utakaosaidia
kuleta maendeleo ya dini ya kiislamu,waumini wake na taifa kwa ujumla
Wakizungumzia mashindanio hayo, baadhi ya waislamu waliofika
katika uwanja wa taifa wamepongeza jitihada zinazofanywa katika
kuawezesha vijana wa kiislamu kuhifadhi Quraan hatua itakayosaidia kuwa na
taifa linamcha mungu na kuondokana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili
Zaidi ya nchi 18 zimehudhuria mashindano hayo wakiwemo pia
viongozi mbalimbali wa serikali, Makamu wa Rais Mstaafu Daktari Mohammed Ghalib
Bilal,baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa akiwemo Katibu mkuu wa CCM Bwana
Abdulrahman Kinana.
Majaliwa watanzania jiepusheni na vitendo au-kauli za kuvunja-amani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment