Jeshi la polisi mkoani Arusha limewashikilia watu wanne akiwemo ofisa
itifaki kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha,Swalehe Mwindadi kwa tuhuma za
kumteka na kisha kumpiga mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Arusha,Lucas
Myovela.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo,Mey 15 mwaka huu,kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Arusha(RPC),Charles Mkumbo amesema kwamba tayari
jeshi lake linawashikilia watuhumiwa hao ambao walikamatwa katika nyakati
tofauti jijini hapa.
Kamanda Mkumbo alisema kwamba watuhumiwa hao walikamatwa juzi usiku na
wameachiwa jana majira ya saa 3 ;00 usiku kwa dhamana na sasa wanaandaa
taratibu za kuwafikisha mahakamani.
Hatahivyo,alisema kwamba mbali na kuwashikilia watuhumiwa hao pia jeshi
hilo linashikilia simu ya mkononi ya ya mmoja wa watuhumiwa kielelezo
kilichotumika katika katika tukio hilo.
Wakati huo huo mwandishi aliyejeruhiwa Myovela amehojiwa na gazeti hili
na kusema kwamba hali yake sio nzuri kwa sasa na bado anaendelea kupata
matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mt Meru.
Mvyovela,alisimulia kwamba katika tukio hilo mbali na watu hao
kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake pia walichukua baadhi ya mali zake
kama simu ya mkononi na fedha.
Hatahivyo,mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani
Arusha(APC),Claud Gwandu ametoa taarifa ya kulaani tukio hilo na kutaka mamlaka
kuwachukulia hatua wanaohusika.
Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari Gwandu alisema kwamba
Myovela hakustahili kuteswa wala kupigwa kwa namna yoyote na endapo kulikuwa na
suala la kijinai wahusika
walipaswa kufuata taratibu na sio kujichukulia sheria mkononi.
Kwa upande wake
,Myovela amesema tukio hilo limemvunjia heshima mbele ya jamii kutokana na wahusika kumdhalilisha kwa kumtesa kwa kipigo akiwa utupu huku wakimpiga picha na kumrekodi kwa kutumia simu zao.
Waliomteka na kumdhalilisha Mwandishi wa habari akiwa Utupu ,Mikononi Mwa Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment