Mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2018/19
umeendelea kuwa moto bungeni baada ya wabunge kuitaka Serikali kuacha kuwabana
wakulima wa mahindi kuuza nje ya nchi.
Mbunge wa Kwela (CCM), Ignas Malocha akizungumza katika
mjadala wa bajeti hiyo bungeni mjini Dodoma leo Mei 15, 2018 amesema, “Siungi
mkono hoja, mkulima wa mahindi ni kama mfungwa, nilitarajia hotuba kama hii
ingekuja na majibu lakini siyaoni.”
“Anauza gunia la mahindi Sh15,000, kitendo hiki
hakiridhishi, hakifurahishi. Waziri (wa Kilimo Dk Charles Tizeba) anasema kuuza
nje hadi apewe kibali apewe kibali, umelima wewee? Kama unaona ni shida yanunue
uyahifadhi, si kazi ya mkulima kutunza. Si sahihi hata kidogo, nazungumza hili
kwa niaba ya wananchi wangu zaidi ya laki nne, inawauma kweli kweli.”
Kuhusu kutotengwa kwa fedha za kilimo cha umwagiliaji,
amesema: “Tuko makini kweli katika kilimo, maendeleo ya viwanda duniani
kote yalianza kwa mapinduzi ya kilimo, lakini kilimo kimewekwa pembeni, mtuulize
sisi tunaoishi na wananchi.
“Mimi nashangaa ndugu
yangu Tizeba najua hii bajeti huiandai nyumbani kwako, hivi wataalamu wanafanya
kazi gani kukusaidia. Hii bajeti hupangi nyumbani kwako wanashauri kitu
gani? hayo madigriii ya kazi gani kumuumiza mkulima.”
Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Dk Damas Ndumbaro amesema,
“Wananchi wa Songea wamenituma nifikishe ujumbe kwa wizara ya kilimo na
Serikali. Wanasema kwao zao la mahindi ni chakula, kwao ni biashara na ni
siasa, hawana viwanda, wanategemea mahindi, mahindi ndio uhai wao
“Lakini sasa hivi wana kilio kikubwa sana, katika
msimu uliopita mbolea haikupatikana kwa wakati, bei ya mbolea ilikuwa
inabadilika kama homa ya vipindi, upatikanaji wa mbolea ulikuwa ni shida na
ukiwanyima mbolea umewaua kabisa.”
Amesema wananchi wanajitahidi kuzalisha, akitolea mfano
Ruvuma mwaka 2016/17 walizalisha tani milioni 1.9, mahitaji na
matumizi kwa mkoa mzima ni tani laki nne hivyo kulikuwa na ziada ya tani
milioni 1.5
Wabunge wahoji wakulima kuzuiwa kuuza mahindi nje ya nchi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment