Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Jacqueline Ngonyani
‘Msongozi’ ametoa chozi bungeni akiitaka Serikali kuwalipa mawakala wa pembejeo
na kuacha kutumia kivuli cha uhakiki wa madeni hayo kutoyalipa
Akichangia bajeti ya kilimo, leo Mei 15, 2018 bungeni,
Msongozi amesema madai hayo yamedumu kwa zaidi ya miaka minne huku baadhi
wakifariki kabla hawajalipwa
“Nashangaa sana mawakala wa pembejeo wanadai miaka minne,
walihudumia wakulima wetu na walikwenda kukopa fedha katika taasisi, ambazo
sasa zinawadai,” amesema Msongozi
Huku akishangiliwa na wabunge, Msongozi amesema, “Serikali
imekuwa inajificha katika kichaka cha uhakiki, kwa nini hawawalipi? Serikali
imekwenda kujificha katika uhakiki, ni uhakiki wa aina gani? Kuna watu wanakufa
bila kupewa fedha zao.”
Msongozi akizungumza kwa sauti yenye kuashiria kulia huku
mkono wake akiupeleka kufuta uso wake, amesema, “katika nchi hii watu
wanatafuta haki zao, kama wameiba kwa nini wasipelekwe mahakamani, kwa nini
hawapewi fedha zao, uhakiki gani, mbona watumishi siku mbili walihakikiwa? Kwa
nini huku katika mawakala hawalipwi fedha zao.”
Amesema kuna kijana alitaka kujinyonga kwa kudaiwa na
taasisi jambo ambalo amesema Serikali ichukue hatua ya kulipa madai kwani wako
mawakala saba wamepoteza maisha.”
Msongozi amekuwa mbunge wa tatu kutoka CCM kutokuunga mkono
bajeti hiyo akitanguliwa na Richard Ndassa (Sumve) na Mashimba Ndaki (Maswa
Magharibi
Mbunge CCM amwaga chozi bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment