Kauli ya mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Katani ya
kufananisha utendaji kazi wa Wizara ya Kilimo na michezo ya kubahatisha maarufu
kama ‘kubeti’ imezua kisaazaa bungeni
Kauli hiyo aliyoitoa leo Mei 15, 2015 katika mjadala wa bajeti
ya wizara hiyo mwaka 2018/19 ulimuinua kwenye kiti Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, Jenista
Mhagama na kusema kauli ya Katani
inawadhalilisha walioko serikalini
Katika maelezo yake Katani amesema hadi leo mawakala
wanaosambaza pembejeo hawajalipwa fedha zao.
Amesema
Sh200bilioni zilizotakiwa kwenda katika mfuko wa korosho hazijaenda kwa
miaka yote kwa ajili ya kukuza zao
“Serikali hii imekuwa ya kubeti beti na kwenye kilimo
imekuwa ikibeti. Fedha za korosho za export levy (ushuru wa mazao yanaouzwa
nje) Sh206bilioni hazilipi. Mnacheza na kilimo, mnawadanganya wakulima wa
korosho,”amesema
Amesema Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amekuwa
akikibeba chama cha ushirika cha Tanecu kwa kukiombea kukopeshwa fedha Sh
200bilioni
Amehoji pia sababu ya msingi ya kumuondoa mkurugenzi wa bodi
ya korosho na kuwaacha watendaji.
“Kwanini
wasingeondolewa watendaji? Hakuna maelezo yanayotosheleza yaliyosababisha
mkurugenzi huyu kuondolewa,”amesema
Hata hivyo, Katani aliombewa utaratibu na Mhagama kuwa lugha
anayoitumia inadhalilisha watu wanaofanya kazi Serikalini kwasababu neno kubeti
lina maana ya kubahatisha
Hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge
kumtaka kufuta maneno hayo lakini Katani akaendelea kufafanua alichokuwa
akikikimaanisha na hivyo kutakiwa na kiti kutoendelea kuchangia
Mbunge CUF adai Serikali ‘inabeti’, azua hekaheka bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment