Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Cecilia Paresso amesema
wakulima wanatakiwa kutambua kuwa adui yao namba moja ni chama tawala, CCM
akisema
haiwezekani asilimia 75 ya Watanzania wanaotegemea kilimo,
lakini imeshindwa kuwasaidia
Amesema Serikali imeshindwa kuwekeza fedha za kutosha
katika kilimo huku kwa upande wa asilimia tano ya Watanzania wanaotumia usafiri
wa anga ndege zimenunuliwa.
Paresso ametoa kauli hiyo leo Mei 15, 2018 katika mjadala wa
bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2018/19 ambapo wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa
Sh170.2bilioni
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), zinaonyesha ukuaji wa sekta ya kilimo mwaka 2011 ilikuwa asilimia 1.9,
mwaka 2012 (3.2), mwaka 2013 (4), mwaka 2014 (3.4), mwaka 2015 (3.2), mwaka
2016 (1.9) na mwaka 2017 kwa asilimia 1.3
“Sekta hii kama itawekeza vizuri itatoa ajira, kuondoa
umasikini na tutafikia hicho mnachosema uchumi wa viwanda, lakini sekta hii
imekuwa haipewi fedha kama inavyotakiwa na fedha tunazozitenga hazifiki,”
amesema Paresso
“Serikali ya Awamu ya Nne inaondoka madarakani iliacha
kilimo kinakua kwa asilimia 3.2, ila hii Serikali ya Awamu ya Tano inayojiita
uchumi wa viwanda, kimeendelea kushuka na kufikia asilimia1.9.”
Amesisitiza, “wakulima wa nchi hii wanapaswa kujua adui yao
ni Serikali, asilimia 75 wanategema kilimo lakini asilimia tano ya Watanzania
wanaotegemea usafiri wa anga wanawepa ndege. Huku ni kuwahadaa wakulima ambao
wanapaswa kujua Serikali ya CCM ndio adui yao.”
Mbunge Chadema aisukumia mzigo CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment