Mbunge wa Viti Maalumu Matha Mlata ametaka Serikali kuachana
kabisa na suala la chapa ya mifugo kwa kuwa inaumiza mnyama bila sababu za
msingi
Hoja hiyo imeungwa mkono na Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye
amesema Wizara imeshindwa kufanya mambo kisomi hata kufananisha wazee wa
zamani ambao waliweka alama mifugo yao na ilitambulika vizuri ingawa hawakuwa
wamesoma lakini walithamini mifugo yao na kuwa na huruma
Katika mchango wake kwa Wizara ya Mifugo, Mlata amesema
mambo yanayofanywa na Wizara hayaonyeshi kabisa kama wizara hiyo inaongozwa na
wasomi
“Kuna msomi gani huko wizarani ambaye anaruhusu kuchoma
vyuma vya moto na kuwachoma wanyama wetu bila sababu za msingi, hivi hakuna
namna nyingine ya kuweka alama hizo?” amehoji Mlata
Mbunge huyo amepinga suala la operesheni akisema haliko
sahihi kwani kuna watu wanaonewa bila sababu za msingi na kwa namna moja
linawanufaisha upande wa serikali tu
Mbunge Innocent Bilakwate amepinga suala la chapa akisema
limeumiza mifugo kwa kiasi kikubwa na halina tija yoyote hivyo akawataka
wataalamu kubuni mbinu nyingine
“Haiwezekani hata kidogo kutumia machuma na kuanza kuwaumiza
mifugo halafu ninyi mnafurahia, hivi hamulioni hilo kuna wataalamu gani huko
jamani,” alihoji
Mbunge wa Namtumbo Edwin Ngonyani amesema katika eneo lake
wameumiza mifugo na chapa hizo hazionyeshi ubora wa aina yoyote zaidi kuacha madonda
yasiyotibika kwa mifugo.
Ngonyani amesema
Namtumbo wameumizwa pia kwa kusababishiwa migogoro baina ya wakulima na
wafugaji baada ya ng’ombe wengi kupelekwa eneo hilo ambalo ni dogo kijiografia
Wabunge waikataa chapa ya mifugo, spika aunga mkono
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment