PM awapa neno wakadiriaji majengo nchin


Dodoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wabunifu na wakadiriaji majengo nchini kuangalia upya viwango vya ada wanavyotoza ili kupanua wigo wa utoaji huduma

Akifungua mkutano wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Nchini (AQRB) leo Mei 18, kwa niaba ya Rais John Magufuli, Majaliwa amesema viwango vya ada vinavyotozwa na wataalam hao ni vikubwa na hivyo kuwafanya wengi kushindwa kuwatumia

“Ada kubwa zinazotozwa katika ukadiriaji majenzi zimewafanya watu kushindwa kutumia huduma na hivyo kuwa na majengo yasiyokidhi viwango,”amesema Majaliwa

Amesema kwa kufanya hivyo kutapanua soko na si kubaki kutegemea kutoa huduma hiyo kwa Serikali

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ,Profesa Makame Mbarawa amesema Wizara yake kwa kushirikiana taasisi nyingine za Serikali inaandaa viwango vya majengo nchini
Amesema kwa viwango hivyo ni kwa ajili ya kusimamia na kuboresha majengo nchini na baada ya kukamilika Serikali  itahakikisha inafuata viwango vinavyotakiwa.

 Kuhusu upungufu wa rasilimali, Profesa Mbarawa amesema katika mwaka wa bajeti 2017/18 Serikali itenga Sh50 milioni kwa ajili ya bodi hiyo lakini katika bajeti ya 2018/19 imeongeza na kufikia Sh100 milioni.
PM awapa neno wakadiriaji majengo nchin PM awapa neno wakadiriaji majengo nchin Reviewed by KUSAGANEWS on May 18, 2018 Rating: 5

No comments: