Jeshi la Magereza nchini limekanusha
taarifa zilizoibuliwa na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kuhusu kukosekana kwa
sare za wafungwa zaidi ya 600, katika gereza la Ruanda alipokuwa amefungwa.
Akizungumza msemaji wa Jeshi hilo
Lucas Mboje, amesema kwamba sio kweli kwamba wafungwa hawana sare na hakuna
kitu kama hiko, isipokuwa kuna mahabusu ambao wapo mule wakiendelea kusubiri
kesi zao, na ndio huenda ambao aliwaona bila sare.
“Hiko kitu hakipo, halafu
asichanganye mambo, kuna mahabusu ambao wao wanajulikana kwa mujibu wa sheria
hawavai sare, sasa asichanganye, mtu akishafungwa inajulikana lazima avae sare,
sasa kuna mahabusu pia, sio kweli kama kuna tatizo la sare hakuna mtu anakosa sare,
hebu fikiria wafungwa karibia 600 kwenye gereza moja wakose sare ni kitu
ambacho hakiwezekani, hiyo itakuwa ni issue nyingine”, amesema Lucas Mboje.
Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu)
alipotoka jela kwa msamaha wa Rais alisema kwamba alilazimishwa kuvaa sare za
jela wakati kuna watu amewakuta gerezani zaidi ya mia 6 wamekosa sare na wapo
mule ndani.
Magereza yamjibu Sugu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment