Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe
Stephen ameagiza mkandarasi aliepewa kazi ya kujenga mradi wa maji katika
kijiji cha Kibwaya kata ya Mkuyuni kurudi mara moja kufanya marekebisho licha
ya mradi kuwa katika kipindi cha matazamio ya kukabidhi.
Baada ya malalamiko hayo ya wananchi
kumfikia Dk. Kebwe na kwenda kujionea amebaini kuwa mradi huo
umejengwa chini ya kiwango huku mkandarasi akiwa amepokea fedha
zote ametoa msimamo wa Serikali kumtaka mkandarasi kurudi kufanya
marekebisho.'
"Nampa siku 14 Mkandarasi
wa mradi huu hata kama yupo chini ya wizara ya maji, lakini hizi ni kazi za
serikali na mimi ndiye Mkuu wa Mkoa. Arudi afanye masahihisho yote. La! sihivyo
atafata nyayo kama yule mwenzake aliyetuharibia barabara ya lami kule kilosa,
mnajua kitu gani nilimfanya" Dk. Kebwe.
Licha ya maagizo hayo pia mkuu huyo
wa mkoa amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa halmashauli ya wilaya ya Morogoro Sudi
Mpili kufuatilia kwa karibu marekebisho ya mradi huo sambamba na kumrudisha
mhandisi wa maji aliyesimamia mradi huo Eng. Steven Mkalimoto ambae kwa
sasa amehamishiwa wilayani Mbozi.
"Siku 14 kama hatafika
kufanya marekebisho atarudi chini ya polisi atasaini asubuhi anakwenda kazini
kila siku mpaka kazi ikamilike. Mkurugenzi Hakikisha sehemu zote maji
yanapovuja hakikisha anaziba na kwenye tenki kuna ufa arekebishe sehemu zote.
Nimepanda kuangalia nimeona maji yanaingi hivyo amalizie marekebisho,"
Dk. Kebwe
Mradi huo ambao unagharimu zaidi ya
shilingi milion 650, ulitakiwa kukamikila tangu mwaka 2015, ukiwa na Tanki moja
pamoja na vituo 15 vya kuchotea maji , ambapo kwa sasa upo katika kipindi cha
matazamio huku wakazi wa eneo hili wakidai baadhi ya vituo havijawahi kutoa
maji
Mkuu wa Mkoa Morogoro ageuka mbogo kisa maji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment