Siku chache baada ya kuondolewa katika Bodi ya Wakurugenzi
ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, mfanyabiashara Herbinder Sethi ameeleza
kusikitishwa kwake na hatua hiyo, huku akisema hautambui uongozi mpya uliowekwa
madarakani
Uamuzi wa kumwondoa Sethi katika bodi ya wakurugenzi ambayo
pia ilimvua uenyekiti wa IPTL, ulifikiwa baada ya kushindwa kushiriki na
kuhudhuria mikutano ya bodi kwa miezi sita mfululizo bila ruhusa, tangu Juni
19, 2017 alipokamatwa na kushtakiwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimsomea Sethi mashtaka 12
ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Dola
22.198 milioni za Marekani (Sh309.5 bilioni
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa wakili wake, Hajra Mungula
iliyotolewa jana kupitia mitandao ya jamii ilisema Sethi hatambui mabadiliko ya
uongozi uliowekwa na kwamba yeye ni mmiliki halali wa IPTL ambayo kimsingi
inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan African Power Solutions (PAP
“Pamoja na kuagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka
za kisheria, Mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hivyo
anapenda kuutaarifu umma wazipuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitokani na mamlaka
halali ya kisheria ya kampuni hiyo,” ilisema taarifa ya Mungula ambaye
alilithibitishia Gazeti la Mwananchi kuitoa
Mungula alisema mabadiliko hayo yamekwenda kinyume na notisi
ya katazo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali la Februari 12, 2018 lenye kumbukumbu
Na. AGS234 lililozuia aina yoyote ya uhamishaji wa mali na umiliki wa mali za
IPTL
“Kimsingi mabadiliko hayo batili yanaathiri na kwenda
kinyume na maelekezo ya Serikali
“Pamoja na kwamba Mwenyekiti bado yuko mahabusu akituhumiwa
kwa mashtaka kadhaa ya jinai, hiyo haiondoi ukweli kuwa IPTL ni kampuni binafsi
yenye wamiliki halali wenye hisa halali, hivyo haiwezekani kwa mtu asiyehusika
na asiye mwanahisa kutangaza mabadiliko ya uongozi bila kufuata taratibu
zilizopo kisheria,” alisema Mungula
Alisisitiza kwamba licha ya Sethi kuwa na mashtaka ya jinai
yanayomkabili, lakini Watanzania wajue bado kampuni hiyo iko chini ya usimamizi
salama wa PAP na kwamba madeni yote, madai ya mali na stahiki zote
zinazohusiana na kampuni hiyo zipo katika mikono salama
Sethi apinga kuenguliwa IPTL
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment