Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson amesema kuwa msiba wa aliyekuwa mbunge wa Kakonko Samson Bilago umepokelewa kwa mshtuko kutokana na wabunge wengi kutokuwa na taarifa za ugonjwa wake.
Dk. Tulia amesema hayo wakati wa ibada ya kuaga mwili wa
marehemu Bilago katika viwanja vya bunge Jijini Dodoma, marehemu aliugua
na taarifa ziliufikia uongozi wa Bunge na taratibu zilianza za kushughulikia
matibabu lakini ni wabunge wachache ambao walikuwa na taarifa hizo.
Marehemu Bilago alifariki Mei 26 mwaka huu katika hospitali ya taifa ya muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya mishipa, mwili wake umeagwa bungeni leo na kuanza safari ya kuelekea Mkoani Kigoma kwaajili ya shughuli ya maziko.
“Wabunge hawakuwa na taarifa za Bilago”-Dk. Tulia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment