Nchi ya Tanzania imetajwa kuwa na
kiwango cha chini cha unywaji wa maziwa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki,
ambapo mtu mmoja hunywa lita 47 kwa mwaka, japokuwa wana Ng'ombe zaidi ya
milioni 30.5.
Akizungumza leo Jijini Arusha Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Lucas Malunde, amesema unywaji huo ni
mdogo ukilinganisha na nchi ya Kenya ambayo kila mtu hunywa lita 110 hadi 111
kwa mwaka.
"Kwa sasa Tanzania inazalisha
lita bilioni 2.4 za maziwa kwa mwaka, kiwango ambacho kidogo ukilinganisha na
idadi kubwa ya ng'ombe waliopo", amesema
Malunde.
Aidha, Malunde amefafanua kuwa licha
ya Tanzania kuwa na ng'ombe wengi lakini kati yao ng'ombe milioni 27 hufugwa
kienyeji na milioni moja ndiyo hufugwa kisasa na kuleta tija ndogo katika
uzalishaji mzuri wa maziwa.
Shirika la Chakula na Kilimo la
Umoja wa Mataifa (FAO), linamtaka kila mtu kwa afya angalau anywe lita 200 za
maziwa kwa mwaka.
Kwa upande mwingine, maonesho ya
kimataifa ya kilimo na maadhimisho ya 21 ya wiki ya maziwa yanayofanyika
kitaifa mkoani Arusha.
Watanzania watajwa kutokunywa maziwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment